Yusufu auliza Peter

Yusufu auliza Peter

Yusufu: Nimesikia ya kwamba Biblia imebadilishwa na kuharibiwa!

Peter: Ngoja kwanza! Kurani inaeleza kuwa Biblia ni neno la Mungu, na pia ya kwamba hakuna mtu yeyote awezae kubadilisha neno la Mungu1 na Biblia yenyewe inatoa ushuhuda wake na uvuvio wake ukithibitisha ya kuwa hakika ni neno la Mungu ambalo limetambuliwa na kuandikwa. Ikiwa mtu yeyote atadai kwamba Biblia imebadilishwa na kuharibika ni heri awe mkarimu, na atoe ushahidi unaofaa, na wayajibu hakika maswali haya:

Lini na mbona ilifanyika? Ilibadilishwa na nani? Basi, iko wapi Biblia ya asili ambayo haikubadiliishwa?

Fatuma: Wakristo wana tafsiri aina nyingi za Biblia.

Grace: Hizi tafsiri za Biblia sio mandishi tofauti bali tafsiri ya maandiko ya Mwanzo. Biblia bila shaka imetafsiriwa katika lugha nyingi tofauti. Mara kwa mara tafsiri ya kisasa ya lugha sawa ziko sasa, kama vile lugha zote huenda na hubadilika kulingana na wakati. Hata hivyo maana na ujumbe1 haujabadilishwa.

Yusufu: Mungu hana Mwana.

Peter: Ninakubaliana nawe ya kuwa Mungu hakuwa na uhusiano wowote wa kimwili na Maria uliyosababisha „kuzaliwa kwa Mwana“. Neno hili „Mwana” kwa hali hii linaonyesha hali ya aina ya kipekee ya uhusiano kati ya Mungu Baba na Yesu Mwana. Yesu alikuwa karibu na Mungu kama vile mtoto alivyo kwa baba yake. Watu hutumia mbinu mbali mbali za maongeo kueleza uhusiano maalum, kwa mfano, neno msafiri kwa kiarabu humaanisha „Mwana wa njia“. Hata hivyo hizi mifano ni vidokezo vya kutuleta karibu ya kumwelewa Mungu, kwa sababu sisi wanadamu tumeshindwa kuelewa kwa hakika Mungu5 ni nani kwa sababu yeye ni roho.

Fatuma: Yesu hawezi kuwa Mungu.

Grace: Yesu ndiye mtu pekee aliyeishi duniani bila dhambi, Yesu hakika alikuwa „Mungu pamoja nasi“ kwa vile alitangaza „Mimi na Baba tu umoja.“ Yesu, kama binadamu, alikuwa mwonekano wa Mungu kwa njia ya kimwili duniani. Hakuna lisilowezekana kwa Mungu akitaka kuja duniani kwa njia kama hii na vile vile aongoze ulimwengu, ni nani atakayemzuia? Wakristo hakika humwamini Mungu mmoja tu, kama vile Biblia inavyofundisha.

Yusufu: Yesu hakusulubiwa.

Peter: Kuna ushahidi kamili wa kusulubiwa kwa Yesu’

  1. Ilitabiriwa na Manabii wa agano la kale.
  2. Yesu mara nyingi alitabiri kifo chake kwa njia iliyo wazi na kwa kinaganaga.
  3. Mashahidi (mitume) walitoa ushuhuda kufuatana na habari hizi.
  4. Wana historia walitoa habari hizi na,
  5. Ushuhuda wa wale ambao maisha yao yalibadilishwa.

Fatuma: Yesu alikuwa nabii wa Waisraeli, lakini Mohammed alikuwa nabii wa ulimwengu wote!

Grace: Wakati wa huduma yake, Yesu aliwafundisha wanafunzi wake, ili kuwatayarisha kwa kazi ya kuleta injili kwa watu wote. Hata hivyo wakati mwingine Yesu aliwahutubia watu wengine ambao walikuwa na hamu ya kusikiliza kuelekea mwisho wa kumalizika kwa kazi yake, aliwapa wanafunzi wake amri kuu na aliwaamuru waende duniani kwote na kuhubiri habari njema kwa watu wote. Hii inaonyesha ya juwa habari njema ya Yesu inaelekezwa kwa watu wote dniani. Tafadhali kumbuka kwamba Kurani4 pia nathibitisha kuenea kwa Yesu duniani!

Yusufu: Kuna Mungu mmoja pekee, sio Mungu watatu kwa fumbo moja au katika utatu!

Peter: Wakristo bila shaka wanaamini kwamba kuna Mungu mmoja! Biblia inamweleza Mungu kama mwenye umbo tatu, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Kuna mifano mingi ya asili ambayo watatu waweza kuwa ndani ya mmoja, kwa mfano, jua lina umbo tatu: mwili, joto na mwangaza. Mafunzo ya Biblia ya utatu yanatusaidia kumjua Mungu vyema, Mungu hupenda kujitambulisha, hii ndio sababu moja ya Yesu kuja duniani ili amfunue Mungu duniani.

Fatuma: Injili ya Barnaba ndiyo „Injili ya ukweli“!

Grace: Wataalamu wamechunguza „Injili“ hii na kuthibitisha ya kuwa imetungwa inje ya Biblia. Kitabu hiki kiliandikwa karne nyingi baada ya hizi Injili zingine nne, katika sehemu nyingi inatofautiana na Biblia na hata Kurani. Kwa mfano, Yesu anachukua jukumu la „mtayarishi“ wa Masiya na Muhammad anaitwa „Masiya“. Kuna makosa kadha ya kijeogorofia na kihistoria ambayo yanathibitisha ya kuwa mwandishi alikosa habari muhimu kadhaa ya hali ilivyokuwa.     

Yusufu: Mohammad ametabiriwa katika Biblia.

Peter: Vifungu vinavyotajwa havizungumzi juu ya Mohammad, jambo hili linaonekana kwa urahisi baada ya uchunguzi wa makini kwenye maandiko yanayohusika. Kutajwa katika agano la kale inaonyesha ya kwamba Yesu ndiye nabii anayekuja, huyo nabii atakuwa kama Musa: Bwana Mungu wako atakuondoshea nabii miongoni mwa ndugu zako kama nilivyo mimi, msikilizeni“ Yesu atimiza usawa kama wa Musa kwa sababu alitoa Agano Jipya, anamjua Mungu uso kwa uso, na alitenda miujiza mikuu na maajabu. Vifungu katika Agano Jipya ambavyo mara kwa mara hutumiwa, vinazungumzia kwa kinaganaga juu ya Roho Mtakatifu, lakini sio Muhammad, kwa mfano Yesu aliposema „atakuwa ndani yenu“ alimaanisha Roho Mtakatifu kwa sababu, yawezekanaje Muhammad, ambaye alikuwa tu binadamu aishi ndani ya wanafunzi wa Yesu?

Fatuma: Njia ya kuingia peponi ni kwa kutenda mema.

Grace: Peponi, ama mbinguni, ni pahali patakatifu ni lazima mtu awe mkamilifu asilimia mia ndipo aweze kufaulu kuingia! Hata tukijaribu kutenda mema kiasi  gani hatuwezi kufikia kiwango cha Mungu na tuwe bila dhambi yoyote. Mungu anajua haya na kwa hivyo anajitolea kutusafisha sisi vikamilifu, kupitia kwa dhabibu ya Yesu Kristo. Kwa hivyo anatumika kama fidia kwa kutulipia dhambi zetu.

Kama unapokea dhabibu hii ya Yesu, utahakikishiwa nafasi Mbinguni, na kisha utashukuru, na kutokana na shukurani kwa Mungu, utaweza kufanya mema.

 

 

Yusufu auliza Peter